Skip to main content

Ujumuishaji jinsia umeongezeka lakini bado kuna pengo- Gilmore

Ujumuishaji jinsia umeongezeka lakini bado kuna pengo- Gilmore

Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa limekuwa na kikao hii leo huko Geneva, Uswisi likiangazia umuhimu wa kujumuisha masuala ya jinsia katika majukumu yake ya kila siku.

Akifungua kikao hicho, Naibu Kamishna Mkuu wa haki za binadamu Kate Gilmore amesema licha ya kuwepo mafanikio kwenye jukumu hilo, ikiwemo kupitisha maazimio, bado kuna pengo kubwa katika kuhakikisha masuala ya jinsia yanapatiwa kipaumbele.

“Wanawake wanapotajwa katika maazimio yanayopitishwa na nchi, wanatambulishwa kimsingi kama waathiriwa wa ghasia zinazohusiana na ukatili wa kingono na kupuuza ghasia nyingine zinazowakumba na vile vile kupuuza jukumu lao kama waleta mabadiliko katika ujenzi wa amani.”