Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Inauma na si haki kumpa mtu hukumu asiyostahili: Mpagi

Inauma na si haki kumpa mtu hukumu asiyostahili: Mpagi

Hebu tafakari, kwa miaka takribani 20 uko jela ukisubiri kunyongwa kwa shutuma za mauaji ambayo hayakufanyika na wala ukuhusika.

Utakuwa katika hali gani ukijua jina lako litaitwa wakati wowote na utatoweka kwenye uso wa dunia. Si hadithi ni hali iliyomsibu Edward Mpagi kutoka Uganda ambaye sasa ana beba bango la kupinga hukumu ya kifo baada ya kupewa msamaha na kutoka jela.

Anazungumza na Flora Nducha katika Makala hii akisimulia ilikuwaje hata roho yake ikawa mkononi..

(MAHOJIANO NA EDWARD MPAGI)