Tathmini itatuwezesha kusaidia wahanga wa tetemeko la ardhi Tanzania-UM

Tathmini itatuwezesha kusaidia wahanga wa tetemeko la ardhi Tanzania-UM

Umoja wa Mataifa nchini Tanzania umesema unatathmini aina ya msaada ambao itatoa ili kusaidia wahanga wa tetemeko la ardhi lililokumba maeneo ya ukanda wa ziwa Viktoria tarehe 10 mwezi huu na kusababisha vifo, majeruhi na uharibifu wa mali. Taarifa zaidi na

(Taarifa ya )

Tetemeko hilo la ukubwa wa 5.9 katika kipimo cha richa, liliathiri zaidi mkoa wa Kagera ambapo watu 16 wamefariki dunia na majeruhi 170 walilazwa hospitalini kwa matibabu.

Umoja wa Mataifa umesema zaidi ya majengo 840 yamebomoka kabisa, mengine zaidi ya 1200 yameharibika, zikiwemo shule tatu.

Hii leo jijini Dar es salaam, serikali ya Tanzania iliitisha kikao cha kuchangia msaada wa wahanga wa tetemeko hilo ambapo mwakilishi mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini humo Alvaro Rodriguez amesema mashirika yao yamejipanga katika utoaji usaidizi hivyo

(Sauti ya Rodriguez)

“Kulingana na kiwango cha uharibifu na tathmini ya mahitaji, bila shaka tutaweza kuleta pamoja mashirika yote yanayoweza kutoa usaidizi, ili yatoe usaidizi. Tunafahamu tayari kuwa baadhi ya vipaumbele itakuwa ni makazi, na vitu ambavyo si vyakula kama vile vifaa vya shule, pia itahitajika chakula kwa wale ambao wanarejea nyumbani.”