Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Upinzani wasitisha ushiriki katika mjadala wa kitaifa DRC

Upinzani wasitisha ushiriki katika mjadala wa kitaifa DRC

Nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC, upande wa upinzani umejitoa kwenye mjadala wa kitaifa kuhusu mustakhabli wa kisiasa nchini humo. Assumpta Massoi na taarifa zaidi.

(Taarifa ya Assumpta)

Katika taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC, MONUSCO, upande wa upinzani umepinga mapendekezo ya kwamba uchaguzi wa rais ufanyike baada ya chaguzi za serikali za mitaa.

Mwezeshaji wa mazungumzo hayo Edem Kodjo amesema kufuatia hali hiyo mashauriano yameanza kati ya wadau ili kuweka mazingira bora kwa kamati husika kwenye mjadala huo wa kitaifa kuweza kufanya kazi.

Mjadala huo wa kitaifa ulianza tarehe Mosi mwezi huu ambapo Umoja wa Mataifa unasema unaamini kuwa mjadala shirikishi ndio njia pekee ya kuwezesha kufanyika kwa uchaguzi halali na wa amani DRC.