Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sielewi kwa nini nchi wanachama hazitoi ushirikiano:Zeid

Sielewi kwa nini nchi wanachama hazitoi ushirikiano:Zeid

Kamishina Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa mataifa Zeid Ra’ad Al Hussein amesema anatiwa hofiu na tabia inayoongezeka ya nchi wanachama kutotoa ushirikiano unaohitajika kwa ofisi yake.

Akizungumza katika ufungunguzi wa kikao cha 33 cha baraza la haki za binadamu kilichoanza leo mjini Geneva, Zeid amesema haelewi ni kwanini baadhi ya nchi hizo hazitaki kutoa fursa kwa wawakilishi maalumu, ofisi yake au mfumo mzima wa ofisi ya haki za binadamu lakini pia kutoishirikisha ofisi hiyo panapostahili. Na kuongeza

(SAUTI YA ZEID)

Ukiukwaji wa haki za binadamu hautokwisha endapo serikali zinazuia fursa za waangalizi wa kimataifa na kuwekeza katika kampeni za umma , ili kukabiliana na matangazo yoyote yasiyohitajika, kinyume chake juhudi za kukataa uchunguzi zinaongeza maswali zaidi , ya nini au kitu gani mnachotuficha?

Amesema ucheleweshaji wa aina yoyote ile kutoka kwa nchi wanachana ni sawa na kukataa kutoa fursa