Skip to main content

Baraza la usalama laelekea Sudan Kusini

Baraza la usalama laelekea Sudan Kusini

Wanachama wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wanaanza ziara yao Sudan Kusini baadaye leo kufuatia kuongezwa muda wa ujumbe wa umoja huo nchini humo, UNMISS.

Kipaumbele cha majukumu ya sasa ni kuimarisha ulinzi wa raia na kuongeza ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa na serikali ya mpito nchini Sudan Kusini.

Wakiwa nchini humo, wajumbe hao watakuwa na mazungumzo na Rais Salva Kiir na viongozi wengine kwenye serikali ya mpito halikadhalika kutembelea maeneo yanayohifadhi raia.

Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Sudan Kusini na mkuu wa UNMISS

Ellen Margaret Loej anataja matarajio yao kutokana na ziara hiyo.

(Sauti ya Ellen)

“Baraza la usalama, kama ilivyo kwetu sisis hapa, limekuwa na wasiwasi mkubwa juu ya kuendelea kwa mapigano katika maeneo mbalimbali ya nchi. Tuna wasiwasi na  hali ya usalama na ya kibinadamu , hivyo ni matumaini yetu kuwa ziara hii itatoa msukumo wa majadiliano ya wazi, juu ya namna bora serikali na Umoja wa Mataifa wanaweza kufanya kazi pamoja kwa manufaa ya watu wa Sudan Kusini.”