Skip to main content

Ban asifu makubaliano mapya ya mpaka kati ya Sudani na Sudan Kusini

Ban asifu makubaliano mapya ya mpaka kati ya Sudani na Sudan Kusini

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Kin Moon ameyakarikibisha makubaliano kati ya Sudan na Sudan Kusini yenye lengo la kuimarisha usalama wa mpaka ambayo yatasaidia kupatia ufumbuzi wa kudumu wa mgogoro wa mpaka kati ya nchi mbili hizo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na msemaji wa Katibu wa Umoja wa Mataifa, makubaliano hayo yanahusu kuanzishwa kwa ukanda usioruhusu shughuli za kieshi kati ya nchi mbili hizo, kupelekwa kwa kundi la pamoja kla kufuatilia makubaliano ya usalama wa mipaka na kuanza kufanya kazi kwa makubaliano ya usalama mpakani.

Bwana Ban amezitaka pande mbili hizo kutoweka masharti yoyote katika utekelezaji wa makubaliano yaliyowekwa saini tarehe 27 mwezi Septemba ikiwemo suala la mafuta na kurejela mwito wake kwa Umoja wa Mataifa kusaidia nchi hizo  katika utekelezaji wa makubaliano hayo.

Ijapokuwa kuzaliwa kwa taifa la Sudan Kusini ni matokeo ya mchakato wa amani wa miaka sita, bado suala la amani kati ya nchi mbili hizo linatatizwa na mapigano ya hapa na pale kwenye mpaka kati yao na hatma ya la eneo lenye mafuta la Abyei ambalo halijapatiwa ufumbuzi.