Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kipindupindu chaendelea kutikisa DRC, chanjo kuanza kutolewa- WHO

Kipindupindu chaendelea kutikisa DRC, chanjo kuanza kutolewa- WHO

Hali ya mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu huko Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo bado si nzuri, limesema shirika la afya duniani, WHO hii leo.

WHO imesema mara nyingi mlipuko huo husalia mashariki mwa nchi hiyo lakini sasa hivi umeenea hadi mji mkuu Kinshasa na kufanya idadi ya waliougua kipindupindu mwaka huu DRC kufikia Elfu 18 idadi ambayo ilikuwa ya mwaka mzima uliopita.

Dokta Dominique Legros kutoka WHO amewaeleza wanahabari mjini Geneva, Uswisi kuwa tayari hatua zimeanza kuchukuliwa kusaidia wizara ya afya na wadau ikiwemo kupeleka wataalamu na vifaa vya tiba na kwamba..

(Dkt. Legros)

“Leo hii ICG imeridhia ombi la chanjo na tutasaidia utekelezaji wa kampeni ya chanjo huko Kinshasa mwisho wa mwezi, ikilenga watu laki tatu. Lengo la kampeni ambayo inalenga maeneo hatarini zaidi ya Kinshasa ambao ni mji mkubwa wenye watu Milioni Tano, ni kudhibiti mlipuko na kuepusha janga kama la miaka mitano iliyopita ambapo visa vilikuwa vingi, halikadhalika vifo.”