Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Madhila ya kusaka maji nchini Uganda

Madhila ya kusaka maji nchini Uganda

MAJI NI AMANI, MAJI NI UHAI , MAJI NI UTU. Hii ni kauli mbiu ya mwaka huu katika maadhimisho ya wiki ya maji duniani ambayo imeanza Agosti 28 hadi Septemba 02 huko Stockholm, Sweden. Katika dunia ya leo ambayo ni kijiji kimoja, upatikanaji wa maji unakwenda sambamba na amani na usalama na ukosekanaji wa maji safi na salama unaathiri dunia nzima kwa njia moja au nyingine. Mabadiliko ya tabianchi , uchafuzi wa mazingira na kuongezeka kwa mahitaji ya maji  kumesababisha ongezeko la  uhaba wa Maji,  hususan katika nchi zinazoendelea.

Ripoti zinasema ni asilimia 2.5 tu ya maji duniani yaliyo salama kunywa na kutumika katika kilimo, na ifikapo mwaka 2050 idadi ya watu duniani inatarajiwa kufikia bilioni 9, na ni chanzo tosha cha kuleta uhasama baina ya watu duniani. Wanaoathirika zaidi ni wanawake na wasichana hususan katika nchi zinazoendelea, kwani ripoti zinasema wanatumia saa milioni 200 kusaka maji, muda ambao wangetumia kujiendeleza au kutunza familia zao.. Je hali ikoje Afrika Mashariki? Tuelekee Uganda ambako mwandishi wetu John Kibego anaangazia madhila wapatayo wanawake kusaka maji nchini humo.

(PACKAGE KIBEGO)