Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban apongeza Gabon kwa uchaguzi wa amani

Ban apongeza Gabon kwa uchaguzi wa amani

Katibu Mkuu umoja wa mataifa  amepongeza Gabon na wananchi wake kwa uchaguzi mkuu wa Jumamosi aliosema umefanyika kwa mpangilio na kwa amani. Taarifa zaidi na Brian Lehander.

(Taarifa ya Brian)

Ban katika taarifa yake pamoja na pongezi hizo amesema  ni matumaini yake kuona haki na uwazi vinaendelea kuzingatiwa kabla ya kutangazwa kwa matokeo rasmi ya uchaguzi.

Amesema ni muhimu kwa pande zote kuheshimu matokeo ya uchaguzi huo, pia  akisisitiza kuwa endapo kutakuwa na kutofautiana katika matokeo ya uchaguzi itakua jambo la busara pande zote kutumia njia sahihi za kisheria na kikatiba.

Katibu Mkuu amemuomba  mwakilishi wake maalum  kwa ukanda wa Afrika ya Kati, Bwana Abdoulaye Bathily kuendelea na jitihada za kushirikiana na wadau ili kumaliza mvutano wowote.