Ban apongeza Gabon kwa uchaguzi wa amani
Katibu Mkuu umoja wa mataifa amepongeza Gabon na wananchi wake kwa uchaguzi mkuu wa Jumamosi aliosema umefanyika kwa mpangilio na kwa amani. Taarifa zaidi na Brian Lehander.
(Taarifa ya Brian)
Ban katika taarifa yake pamoja na pongezi hizo amesema ni matumaini yake kuona haki na uwazi vinaendelea kuzingatiwa kabla ya kutangazwa kwa matokeo rasmi ya uchaguzi.
Amesema ni muhimu kwa pande zote kuheshimu matokeo ya uchaguzi huo, pia akisisitiza kuwa endapo kutakuwa na kutofautiana katika matokeo ya uchaguzi itakua jambo la busara pande zote kutumia njia sahihi za kisheria na kikatiba.
Katibu Mkuu amemuomba mwakilishi wake maalum kwa ukanda wa Afrika ya Kati, Bwana Abdoulaye Bathily kuendelea na jitihada za kushirikiana na wadau ili kumaliza mvutano wowote.