Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

China imejitahidi kupambana na umasikini lakini bado ina kibarua:Alston

China imejitahidi kupambana na umasikini lakini bado ina kibarua:Alston

Uchina imepiga hatua katika kupambana na umaskini lakini bado inahitaji kuweka mikakati kabambe inayoweza kutumiwa na wananchi wanapodhulumiwa katika shughuli zinazohusika na maendelelo.

Hayo ni kwa mujibu wa Mwakilishi maalum wa Umoja wa mataifa kuhusu kutokomeza umasikini Philip Alston. Amesema pamoja na kwamba China imepga hatua katika kupunguza umaskini lakini bado chama tawala cha kikomunisti kinakumbwa na changamoto nyingi kama vile tofauti kubwa katika usawa wa maisha,uharibifu wa mazingira,ukuaji pole pole wa uchumi na shida ya utekelezaji wa utawala wa sheria lakini akaipongeza China kwa dhamira yake ya kumaliza umaskini na kuunda nchi yenye usawa.

Rais Xin Jinping ameahidi kumaliiza umaskini nchini  China ufikapo mwaka wa 2020 akisema hakuna atakaewachwa nyuma na hata wanaoishi mashambani watafaidika katika mpango huo. Lakini kwa mujibu wa Mwakilishi Alston, pande kubwa la haki za kibinadamu halijapewa kipao mbele.