Skip to main content

Bloomberg ateuliwa balozi wa dunia dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza

Bloomberg ateuliwa balozi wa dunia dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza

Shirika la afya duniani, WHO limemtangaza Michael R. Bloomberg, kuwa balozi wake ulimwenguni wa magonjwa yasiyoambukiza, NCD.

Magonjwa hayo ikiwemo yale ya moyo, kiharusi, kisukari na mfumo wa hewa pamoja na ajali husababisha vifo vya watu Milioni 43 duniani kote kila mwaka.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dkt. Margaret Chan amesema Bwana Bloomberg kwa muongo uliopita amekuwa akishirikiana na shirika hilo kwenye harakati za kudhibiti matumizi ya tumbaku, usalama barabarani na udhibiti wa watu kuzama kwenye maji.

Kwa mantiki hiyo amesema ana furaha kubwa kumteua kuwa balozi wa dunia kwa NCDs akisema hatua hiyo itawezesha WHO kuimarisha afya ya umma na kushughulikia changamoto za kudhibiti magonjwa hayo yasiyoambukiza.

Akizungumzia uteuzi wake, Bwana Bloomberg amesema ni heshima kubwa na kwamba atashirikiana na miji na majiji kote ulimwenguni kuboresha afya ya umma.