Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ridhio la Somalia kuwa na tume ya haki za binadamu ni nuru- Nyanduga

Ridhio la Somalia kuwa na tume ya haki za binadamu ni nuru- Nyanduga

Kitendo cha Rais wa Somalia kutia kuwa saini kuwa sheria muswada wa tume ya haki za binadamu nchini humo ni hatua muhimu katika kulinda na kutetea haki za binadamu nchini humo.

Hiyo ni kauli ya mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu Somalia, Tom Bahame Nyanduga, aliyoitoa wakati akihojiwa na idhaa hii kuhusu hatua hiyo ya Somalia akisema..

(Sauti ya Nyanduga-1)

Bwana Nyanduga amesema si hatua ndogo kwa kuzingatia safari ya Somalia ya kujenga demokrasia iliyoanzia serikali kutekeleza shughuli zake kutoka Nairobi, Kenya hadi kurejea Mogadishu na kwamba..

(Sauti ya Nyanduga-2)