Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Licha ya madhila, watoto bado wana matumaini- Zerrougui

Licha ya madhila, watoto bado wana matumaini- Zerrougui

Idadi kubwa ya watoto walioko maeneo ya vita bado wana matumaini licha ya maisha yao kusambaratishwa na mizozo inayoanzishwa na watu wazima. Rose-Mary Musumba na ripoti kamili.

(TAARIFA YA ROSE)

Ni kauli ya msaidizi  wa Katibu Mkuu kuhusu watoto maeneo ya vita Leila Zerrougui aliyotoa wakati akihojiwa na Radio ya Umoja wa Mataifa baada ya maonyesho ya picha za watoto walioko kwenye mizozo yaliyopatiwa maudhui ya “pindi nikikua mtu mzima!”

Maonyesho hayo yaliyoratibiwa na ofisi ya uratibu wa misaada ya kibinadamu OCHA yalikuwa na picha za watoto kuanzia Afrika hadi Mashariki ya Kati.

Bi. Zerrougi ambaye naye amekulia kwenye maeneo ya mzozo amenukuu watoto hao ambao amesema hawajakata tamaa na wanataka kuwa watu bora zaidi kuliko kizazi cha sasa, wakisema….

(Sauti ya Zerrougui)

“Askari si watu wema, walimuua kaka yangu, lakini nataka kuwa askari ili kupambana nao! Kulinda wananchi,  mwingine alisema. Ningependa kuwa polisi ili kusimamia haki. Walitueleza kuwa wangependa kusaidia wazazi wao,kulinda jamii zao, kwenda shule hata kama hawaendi shule!  Wanapitia machungu lakini bado wanatuambia wangalipenda kuweka na dunia bora.”