Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nitachangia kunusuru dunia dhidi ya mabadiliko ya tabianchi:Espinosa

Nitachangia kunusuru dunia dhidi ya mabadiliko ya tabianchi:Espinosa

Katibu Mtendaji wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (UNFCCC) Patricia Espinosa amesema atafanya kila awezalo ikiwamo kutoa usaidizi kwa wadau wa masuala ya mabadiliko ya tabianchi kuhakikisha mkataba wa Paris unaleta ahueni kwa sayari dunia. Flora Nducha na maelezo kamili.

( TAARIFA YA FLORA)

Katika mahojjabnao na redio ya Umoaj wa Mataifa, Bi Espinosa ambaye ameteuliwa mwezi Mei kushika wadhifa huo, amesema kwa kutambua kuwa mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabanchi unahitaji msukumo, UM lazima usaidie serikali katika mchakato wa kuutekeleza ikiwamo sheria na miradi ya nchi.

Kuhusu uhusiano kati ya malengo ya maendeleo endelevu SDGs na mabadiliko ya tabianchi, amesema jamii na jumuiya ya kimataifa lazima zioanishe dhana mbili hizo huku akisisitiza kuwa.

( SAUTI ESPINOSA)

‘‘Tunahitaji kuzalisha mifumo, mifumo ya kisheria, ya kitaasisi na sera zinazohitajika ilikuruhusu nchi ziwe na michakato ya kimuundo inayohitajika, Kwahiyo, hili ni eneo ambalo litahitaji rasilimali nyingi za UNFCCC ambapo nami nitajitolea katika hilo pia.’’