Skip to main content

Ban ashtushwa na ripoti kuhusu UNMISS atangaza uchunguzi huru

Ban ashtushwa na ripoti kuhusu UNMISS atangaza uchunguzi huru

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameeleza kushtushwa kwake na matokeo ya awali ya uchunguzi uliobaini kuwa ujumbe wa umoja huo Sudan Kusini, UNMISS haukuchukua hatua sahihi kuzuia shambulio dhidi ya hoteli moja mjini Juba, lililoenda sambamba na mtu mmoja kuuawa, raia wengine kupigwa na kubakwa na watu waliokuwa wamevaa sare.

Uchunguzi huo wa awali umefanywa na UNMISS ambapo Ban kupitia taarifa ya msemaji wake ameamua kuanzisha uchunguzi huru ili kupata ukweli wa tuhuma hizo alizosema ni nzito.

Amesema uchunguzi huo huru unalenga kubaini mazingira yaliyosababisha matukio hayo sambamba na kutathmini hatua zilizochukuliwa na UNMISS.

Naye Eugene Owusu ambaye ni mratibu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudani Kusini anasema.

(Sauti ya Eugene)

“Kulaani kile ambacho ni tabia isiyokubalika iliyofanywa na mtu mmoja mmoja., na ninataka kutumia fursa hii kutoa wito kwa mamlaka kufanya uchunguzi wa kina wa suala hili, hatuwezi kuruhusu ukwepaji sheria kuendelea.”