Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pande husika kwenye mgogoro Ukraine lazima zilinde raia:Zeid

Pande husika kwenye mgogoro Ukraine lazima zilinde raia:Zeid

Kamishina Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Ra’ad Al Hussein Jumatano amezitaka pande zote katika mgogoro wa Mashariki mwa Ukraine kutoa kipaumbele kwa ulinzi wa raia, na kuchukua hatua za kupunguza hali ya mvutano inayoongezeka , akionya kwamba idadi ya vifo kwa raia imeongezeka sana miezi miwili iliyopita.

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imeorodhesha visa 69 vya raia Mashariki mwa Ukraine mwezi Juni ikiwemo vifo 12 na majeruhi 57 . Idadi hiyo ni karibu mara mbili ikilinganishwa na mwezi Mei na ni idadi kubwa zaidi tangu mwezi agost mwaka 2015.

Na mwezi Julai idadi ikaongezeka zaidi imesema ofisi hiyo, na kuonya kwamba hali hiyo inatia hofu na raia wanalazimika kukimbia, kama anavyofafanua Ravina Shamdasani msemaji wa ofisi ya haki za binadamu...

(SAUTI YA RAVINA)

“Pande zote katika mgogoro ni lazima zichukue hatua malaumu kuhakikisha kwamba raia wanalindwa  na athari za vita, mkuu wa haki za binadamu pia ameitaka serikali ya Ukraine kuridhia mkataba wa Roma wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu, kwa sababu mkataba huo utawezesha  katika vita hivyo kufuatiliwa kwa wajibu binafsi.”