Tumenuia kutokomeza homa ya ini ifikapo 2030: Tanzania

28 Julai 2016

Tarehe 28 mwezi Julai kila mwaka dunia inaadhimisha Siku ya Ugojwa wa Homa ya Ini. Ugonjwa huu unaongoza kwa maambukizi ukilinganishwa na virusi vya Ukimwi, lakini wengi hawautambui hata kuchukua hatua dhidi yake. Hii ni kauli ya shirika la afya ulimweguni WHO linalozihamasisha nchi wanachama kuchua hatua za tiba na elimu hima.

Kwa mujibu wa WHO watu milioni 40 Duniani kote wameambukizwa homa ya ini aina B na C, ikiwa ni mara 10 zaidi ya watu wanaoishi na VVU.

Hali ikoje Tanzania? Hilo ni swali  ambalo Joseph Msami katika mahojiano amemuuliza  Dkt. Angelina Sijaona, Mratibu wa ugonjwa wa homa ya ini katika wizara ya afya nchini humo ambaye pia anafanya kazi na shirika la afya ulimweguni WHO katika kuhakikisha gonjwa hilo linatokomezwa.

Dk Sijaona pia anaeleza miakakati yaTanzania katika kutokomeza homa ya ini, lakini kwanza ni takwimu za wagonjwa.

( SAUTI MAHOJIANO)

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter