Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa UNCTAD 14 wafunga pazia Nairobi Kenya

Mkutano wa UNCTAD 14 wafunga pazia Nairobi Kenya

Mkutano wa 14 wa Kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD, umefikia ukingoni leo kwa wanachama 194 kupitisha maafikiano ya Nairobi. Flora Nducha na ripoti kamili.

(Taarifa Assumpta)

Natts....

Sherehe tangulizi za kufunga mkutano huo wa siku Sita, zilianza saa 10 alasiri kwa ngoma za kitamaduni..

Mwenyekiti wa Mkutano Balozi Amina Mohammed akaongoza kikao cha mjadala kupitia nyaraka mbali mbali tayari kupitishwa ikiwemo ile ya kuongoza nchi Mwenyekiti Kenya katika kufuatilia makubaliano yaliyopitishwa, halikadhalika nyaraka ya kikao ikiitwa Nairobi Maafikiano.

Wajumbe waliridhia kupitishwa kwa Nairobi Maafikiano ambapo awali Balozi Amina akizungumza na wanahabari amesema..

(Sauti Amina)

Mkutano wa UNCTAD hufanyika kila baada ya miaka minne.