Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

DRC imejitahidi katika vita dhidi ya ukatili lakini kazi bado ipo:Zeid

DRC imejitahidi katika vita dhidi ya ukatili lakini kazi bado ipo:Zeid

Kamishina mkuu wa Umoja wa mataifa wa haki za binadamu Zeid Raad Al-Hussein amesema Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC inajitahidi katika vita dhidi ya ukaliti na unyanyasaji lakini bado kazi ipo. Joshua Mmali na taarifa zaidi

(TAARIFA YA JOSHUA)

Zeid ambaye yuko ziarani nchini DRC ameyasema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Kinshasa kwenye makao makuu ya mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO.

Ameipongeza nchi hiyo kwa hatua waliyofikia katika mapambano dhidi ya ukatili, lakini akaonya kwamba mafanikio hayo yako hatarini hasa wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu.

Ameongeza kuwa ofisi yake imepokea ripoti kadhaa za ukiukwaji wa haki za binadamu unaohusiana na mchakato wa uchaguzi, vikiorodheshwa visa 800 vya unyanyasaji kwa mwezi Mei na juni pekee mwaka huu, na asilimia kubwa ya visa hivyo vinahusua makabiliano na waandamanaji , wanasiasa na wafuasi wa upinzani. Na kuongeza

(SAUTI YA ZEID)

“Nimekuwa na mkutano wa waathirika wa ukkukaji wa haki za binadamu , na natarajia katika siku chache zijazo , kujadili masuala yote yanayohusu haki za binadamu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na maafisa wa serikali”