Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wagombea nafasi ya Katibu Mkuu UM kuambiwa matokeo ya kura isiyo rasmi:

Wagombea nafasi ya Katibu Mkuu UM kuambiwa matokeo ya kura isiyo rasmi:

Wagombea 12 wanaowania nafasi ya kuwa Katibu Mkuu ajaye wa Umoja wa Mataifa , wataelezwa matokeo ya kura ya kwanza isiyo rasmi ya baraza la usalama la Umoja wa mataifa ili kupunguza idadi. Hayo ni kwa mujibu wa Rais wa baraza la usalama, Koro Bessho, ambaye alizungumza kidogo na waandishi wa habari baada ya kura hiyo ya Alhamisi asubuhi kwenye makao makuu ya Umoja wa mataifa.

Besho ameelezea umuhimu wa kuwa na kura hiyo ya kwanza isiyo rasmi.

(SAUTI KORO BESHO)

"Ni katika kuwajulisha wagombea nafasi yao katika mchakato. Wagombea watajulishwa matokeo kupitia wawakilishi wao wa kudumu wa nchi wanachama husika".

Rais wa Baraza kuu, Morgens Lykketoft, amepeleka barua kwa mabalozi akieleza kwamba kushindwa kutoa taarifa zaidi ya kusema kura isiyo rasmi imefanyika “haitoshelezi matarajio ya uanachama na viwango vipya vya ukweli na uwazi.