Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

#UNCTADYouth: Tuache kulaumiana, tuchukue hatua kuokoa vijana- Alhendawi

#UNCTADYouth: Tuache kulaumiana, tuchukue hatua kuokoa vijana- Alhendawi

Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu vijana, Ahmad Alhendawi amesema wakati umefika wa kuacha kurushiana lawama kuhusu chanzo cha ukosefu wa ajira kwa vijana duniani na badala yake hatua stahili zichukuliwe ili kuweza kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu. Ripoti ya Assumpta Massoi kutoka Nairobi, Kenya inafafanua zaidi.

(Taarifa ya Assumpta)

Kwa siku tatu vijana kutoka pande mbali mbali za dunia wanakutana jijini Nairobi, kwenye jukwaa la kwanza kabisa la vijana kuenda sambamba na mkutano wa  kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD.

Ahmad Alhendawi, baada ya kuzungumza nao, ukosefu wa ajira ukiwa tatioz kubwa, amesema, kila mtu anarushia lawama mwenzake; waajiri wanadai vijana hanawa stadi, vijana wanasema hawapati mitaji, sekta binafsi inadai sera si rafiki..vijana wakisalia kuwekwa rehani kutokana na ukosefu wa uratibu wa mipango...hivyo...

(Sauti ya Alhendawi)

"Tunapaswa kuwaleta hawa wadau pamoja; vyuo vya elimu, sekta binafsi na wadau wa biashara pamoja na serikali na wadau wa maendeleo ili wazungumze pamoja ili hatimaye sera wanazobuni ziwekeze zaidi kwa vijana."

Sambamba na hilo, Mjumbe huyo maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu vijana amesema serikali ziwe tayari kusikiliza vijana, badala ya serikali kusalia kutoa mihadhara kwa vijana bila kusikiliza mahitaji au mapendekezo ya suluhu za changamoto zinazowakabili.