Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwandishi Alfred Taban anayeshikiliwa Sudan Kusini aachiliwe:UM

Mwandishi Alfred Taban anayeshikiliwa Sudan Kusini aachiliwe:UM

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa kuhusu uhuru wa maoni na kujieleza , David Kaye,leo ameitaka serikali ya Sudan Kusini kumwachilia mara moja Alfred Taban, mwaandishi wa habari nguli na mhariri mkuu wa gazeti la Kiingereza la kila siku nchini humo, Juba Monitor.

Bwana. Taban alikamatwa Julai 16 na mawakala wa usalama wa taifa , siku moja baada ya kuchapicha Makala gazetini iliyokuwa ikitoa wito wa kuenguliwa kwa Rais , Salva Kiir, na makamu wa Rais, Riek Machar, ikiwakosoa kwa kushindwa kutekeleza mkataba wa amani uliotiwa saini mwezi agosti 2015. Hadi sasa mwandishi huyo anashikiliwa bila mashitaka yoyote.

Kaye amesema ni muhimu saana kwa nchi inayosaka kuwa na amani na utulivu kuchukua hatua za kuchagiza uhuru wa kujieleza kwa kila mtu, na hatua zozote zashinikizo kwa waandishi habari ni ishara ya hatua za ukandamizaji ambazo Sudan Kusini haipaswi kuzichukua.

Dkt. David Carson ni Mkurugenzi wa programu ya utafiti wa hali ya hewa duniani.

“Kwa wakati huu, tumeshangazwa na tulichoona katika miezi sita ya kwanza, lakini pia tupo mahali tunapoweza kuanza kusema, kutokana na rekodi za miezi sita ya kwanza, tunachoweza kutabiri kwa mwaka huu mzima. Siyo tu kwamba hiki ni kiwango juu ya wastani, lakini ni juu ya rekodi. Kiwango joto mwaka huu kimezidi rekodi saba za awali.”