Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afrika ibadili mbinu za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi-Kamau

Afrika ibadili mbinu za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi-Kamau

Mkutano wa ngazi ya juu kuhusu madhara ya El Niño na hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ukianza leo mjini New York, bara la Afrika linapaswa kuongeza uwezo wa kukabliana na madhara hayo.

Katika mahojiano na idhaa hii, mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya El Niño na mabadiliko ya tabianchi, Balozi Macharia Kamau amesema mabadiliko ya tabianchi yameongeza kasi ya El Niño na La Niña, hivyo kwa bara la Afrika.

(SAUTI KAMAU)

Kadhalika amesema jamii inapaswa kuongezewa uelewa wa kutambua na kukabiliana na madhara ya mabadiliko ya tabianchi hususani katika maeneo ambayo yameathirika zaidi.