Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Karibu watoto robo milioni wana utapia mlo mkali Borno, Nigeria

Karibu watoto robo milioni wana utapia mlo mkali Borno, Nigeria

Karibu watoto robo milioni wana utapia mlo mkali kwenye jimbo la Borno , Kaskazini Mashariki mwa Nigeria na wanakabiliwa na hatari kubwa ya vifo.Flora Nducha na taarifa zaidi.

(TAARIFA YA FLORA)

Hayo yamesemwa leo jumanne na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, wakati madhila ya kibinadamu yaliyosababishwa na mashambulizi ya Boko Haram yakiendelea.

Kwa mujibu wa UNICEF wakati huu ambapo fursa ya kufikia maeneo mengi zaidi kwa misaada ya kibinadamu ikipatikana ndio hali hali ya utapia mlo imejulikana.

UNICEF inasema msaada wa haraka unahitajika kukabili na dharura hii. Kati ya watoto 244,000 wanaoungua utapia mlo kwenye jimbo la Borno, inakadiriwa kuwa 49,000 ikiwa ni mtoto mmoja kati ya watano watakufa kama hawatofikiwa na matibabu haraka. Manuel Fontaine ni mkurugenzi wa Kanda ya Afrika Magharibi na Kati wa UNICEF

(SAUTI YA FONTAINE)

"Mara moja ambayo nakumbuka ni pale nilipotembea kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani Dikwa ambako kuna takriban watu elfu sabini na kumuona mtoto wa miaka miwili ambaye ana uzito wa kilo tano tu ."