Wakati tukimuenzi Mandela, tupambane na unyanyasaji na ubaguzi:Stevie Wonder

18 Julai 2016

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya amani, ambaye pia ni mwanamuziki nguli, Stevie Wonder amesema leo hii tunapomkumbuka na kumuenzi Nelson Mandela , tukumbuke yale aliyoyapigania.

Akizungumza katika hafla maalumu ya kumuenzi Mandela kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, amesema Mandela alifungua njia ya kupambana na vitendo vyote vilivyo kinyume na utu na katika kufuata nyazo zake ni lazima kupambana na upingaji wa demokrasia, ukiukwaji wa haki za binadamu, chuki, ubaguzi wa rangi na kutovumiliana.

Ameongeza kuwa kwake yeye siku hii ni muhimu sana kwa sababu Mandela

(SAUTI YA STEVIE WONDER)

“Aliendeleza ari kwa wakati wote akisema tuungane, na la muhimu zaidi alisema tushikamane na tuwe dunia yenye umoja. Na kama nyimbo zangu zinahamasisha watu, na endapo naweza kuwa muziki kama ari ya mtu huyo muhimu alivyokuwa Nelson Mandela, basi nini kitakosekana wasiposikia muziki wangu siku chache, wiki chache , au miezi michache”?

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter