Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Juhudi zaidi zahitajika kukabiliana na ulanguzi wa madawa na uraibu: UNODC

Juhudi zaidi zahitajika kukabiliana na ulanguzi wa madawa na uraibu: UNODC

Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi inayohusika na madawa na uhalifu, Yuru Fedotov, amesema kuwa biashara haramu katika dawa za kulevya ni tishio kubwa kwa afya ya umma, uongozi mzuri na maendeleo endelevu magharibi na kati mwa bara Asia, na kwingineko duniani.

Bwana Fedeotov amesema hayo wakati akikutana na Waziri wa Afghanistan anayehusika na kukabiliana na madawa haramu.Din Mohammad Maboarez Rashidi.

Amesema kuna haja ya kukabiliana na tatizo linalozidi kuongezeka la matumizi ya madawa ya kulevya nyumbani, akiongeza kuwa sasa kuna zaidi ya watu milioni moja nchini Afghanistan ambao ni waraibu wa afyuni, ambalo ni janga la kitaifa. Amesema ni lazima kutoa usaidizi kwa watu hao, wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto, katika kutoa matibabau na kuzuia matumizi.

Bwana Fedotov amesema matokeo ya utafiti kuhusu uzalishaji na matumizi ya afyuni nchini Afghanistan yanakatisha tamaa, lakini pia amezingatia ufanisi ulofikiwa katika kuimarisha vyombo vya dola vya kupinga madawa haramu. Asilimia 90 ya uzalishaji wa afyuni hufanyika katika mikoa 9 ya Afghanistan.