Skip to main content

Ban asema anafuatilia kwa karibu hali Uturuki

Ban asema anafuatilia kwa karibu hali Uturuki

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amesema anafuatilia kwa karibu, na kwa masikitiko makubwa hali nchini Uturuki.

Taarifa ya msemaji wake, imesema wakati huu wa sintofahamu nchini Uturuki, Katibu Mkuu anatoa wito kuwepo utulivu, kujizuia, na kusiwepo vitendo vya ghasia.

Aidha, Ban amesema kudumisha haki za msingi za binadamu, ukiwemo uhuru wa kujieleza na kujumuika, ni muhimu.

Ban amesisitiza kuwa kuingilia kati kwa masuala ya serikali yoyote ile kijeshi hakukubailiki, na kwamba itakuwa vyema iwapo utawala wa kiraia na sheria utadumishwa kwa misingi ya kidemokrasia.