Umewadia wakati wa sauti za wahamiaji kusikika:IOM

Umewadia wakati wa sauti za wahamiaji kusikika:IOM

Wiki hii shirika la kimataifa la uhamiaji limetoa ripoti kuhusu uhamiaji na wahamiaji duniani, ikijikita katika lengo moja kubwa, kuhakikisha sauti ya wahamiaji inasikilizwa.

Ripoti hiyo inasema wahamiaji kwa mamilioni duniani wanajikuta katika hali ngumu iwe ni katika kutendewa haki, kutimiza mahitaji na hata kushirikishwa katika maamuzi, sababu ni kwamba sauti yao haijapewa nafasi.

Shirika hilo sasa linasema umefika wakati sauti za wahamiaji sio tuu zisikizwe ila zitiliwe maanani na kufanyiwa kazi.

Nimeketi na afisa wa habari na mawasiliano wa IOM Jumbe Omari Jumbe kuichambua ripoti hiyo na kupata ufafanuzi kwa nini sauti za wahamiaji zina umuhimu wa kusikika

(MAHOJIANO NA JUMBE OMARI JUMBE)