Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mamilioni ya vijana wana ajira zisizokidhi mahitaji: ILO

Mamilioni ya vijana wana ajira zisizokidhi mahitaji: ILO

Kulekea siku ya ujuzi kwa vijana duniani Julai 15, Shirika la kazi duniani ILO limesema licha ya takwimu za ajira kwa vijana kuongezeka, wasiwasi umesalia juu ya idadi ya vijana ambao wana kazi lakini ni masikini. Joshua Mmmali na taarifa zaidi.

( TAARIFA YA JOSHUA)

Katika mkutano wa kimataifa kuhusu kazi hivi karibuni ILO imejadlili hadhi za kazi kwa vijana mbalimbali ambapo mtaalamu wa ajira katika ILO Sera Elda anasema.

( SAUTI SERA)

‘‘Vijana milioni 235 hususani katika nchi zinazoendelea wanafanya kazi lakini katika ujira mdogo. Hawa ni masikini wanaofanya kazi. Hapa tunazungumzia idadi kubwa ya vijana’’

Takwimu zinaonyesha kuwa wakati wa mkwamo wa kiuchumi duniani vijana bilioni moja na laki mbili kote duniani walio kati ya umri wa miaka 15 hadi 24 walikuwa hawana ajira.