Skip to main content

Mji mkongwe Djenné nchini Mali hatarini kutoweka

Mji mkongwe Djenné nchini Mali hatarini kutoweka

Kamati ya urithi wa dunia imeuongeza mji mkongwe wa Djenné nchini Mali katika orodha ya maeneo yaliyo hatarini kuondolewa katika urithi wa dunia kutokana na ukosefu wa usalama.

Hatua hiyo inaathiri eneo hilo na kuzuia utekelezaji wa hatua za ulinzi wa eneo hilo la urithi wa dunia nchini Mali ambapo kamati katika taarifa yake imeelezea kusikitishwa kuhusu mji huo ambao uo katika eneo lililoathiriwa na machafuko.

Kamati imeitaka jumuiya ya kimataifa kusaidia Mali katika juhudi za kuhakikisha ulinzi wa eneo la mji Djenné.

Mji huo mkongwe uliogunduliwa tangu mwaka wa 250 B.C ulikuwa kitovu cha soko na kiuongo muhimu katika baiashara ya dhahabu kwenye ukanda wa Sahara.