Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mafua ya ndege H5N1 yasambaa Afrika Magharibi, watu watakiwa kuwa waangalifu:FAO

Mafua ya ndege H5N1 yasambaa Afrika Magharibi, watu watakiwa kuwa waangalifu:FAO

Cameroon imekuwa taifa la katribuni kubaini mafua ya ndege aina ya H5N1. Nchi zote Afri,ka Magharibi na kati sasa ziko katika tahadhari wakati homa ya mafua hiyoi ikiendelea kusambaa limesema shirika la chakula na kilimo FAO.

Mafua hayo yanaweza kuambukizwa kwa binadamu na kusababisha vifo, na yanaua haraka sana kuku.

Hivi karibuni yamethibitishwa katika shamba la kuku nchini Cameroon na kufanya ufugaji wa kuku katika taifa hilo na mataifa jirani kuwa katika hatari kubwa.

Mlipuko huo unafanya idadi ya nchi zinazokabiliana na mafua hayo ya ndege Afrika ya Magharibi na Kati kufikia sita zikiwemo Burkina Faso, Ivory Coast, Ghana, Niger na Nigeria.

Hii ni mara ya kwanza maradhi hayo kupatikana Afrika ya Magharibi na KJati tangu mwaka 2006.