Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zaidi ya wakimbizi 300 wapokewa Uganda kufuatia mapigano Juba

Zaidi ya wakimbizi 300 wapokewa Uganda kufuatia mapigano Juba

Licha ya kuripotiwa vizuizi vingi na kufunguliwaa kwa mipaka rasmi baina ya Uganda na Sudan Kusini, wakimbizi zaidi ya 300 wanaohofia uhai wao tayari wameingia Uganda kupitia njia zisizo rasmi na vichakani. John Kibego na taarifa zaidi.

(TAARIFA YA KIBEGO)

Shirika la Umoja wa Matifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, Uganda limesema wakimbizi 226 walipokewa jana kando ya 126 waliopokewa Jumapili na 73 waliofika Jumamosi.

Baadhi yao tayari wamehamishwa hadi kweny kambi ya Kiryandongo  iliopo wilayani kiryandongo.

Chalrles Yaxley ni msemaji wa UNHCR, Uganda.

(Sauti ya Charles)

“Tunaarifiwa kwamba mipaka baado imefungua, lakini kuna wakimbizi wanaovuka mpaka kupitia njia zisizo rasmi. Na kuna iwengine ambao wanahitaji kuvuka. Jumamosi peke tulikuwa na tisini na tano.

Wakati huohuo, chini ya maagizo ya Raisi Jeshi la Wanainchi wa Uganda, UPDF limeingia nchini Sudan Kusini kwa ajili ya kukwamua maelfu ya raia wake waliokutua na mapigano nchini humo.