Skip to main content

Juhudi za kurejesha utulivu Sudan Kusini zaendelea: Ladsous

Juhudi za kurejesha utulivu Sudan Kusini zaendelea: Ladsous

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limekuwa na mkutano kuhusu hali ya machafuko nchini Sudan Kusini ambapo mkuu wa opreseshni za ulinzi wa amani katika Umoja wa Mataifa Hervé Ladsous amelihutubia baraza hilo. FloraNducha na taarifa kamili.

( TAARIFA YA FLORA)

Kiongozi huyo amesema hali nchini Sudan Kusini inatia hofu hasa kwa kuzingatia kuwa zaidi ya watu 270 wamefaraiki dunia, mapiganao yanaendelea na takribani watu 42,000 hawana makazi, wengine 35,000 wakiwa katika kambi za UM.

Ladsous amesema juhudi za upatanishi hususani hatau za dharura za kusitisha mapigano hima zinaendelea zikijuimuisha viongozi wa ukanda wa kwa uratibu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS.

Amesema la kusikitisha zaidi mashambulizi yanatekelezwa hata katika maeneo ambapo UM umehifadhi wakimbizi hatua iliyosababisha vifo vya watu wanane wakiwamo walinda amani wawili na mfanyakazi mmoja wa UM huku wengine saba wakijeruhiwa.

( SAUTI LADSOUS)

‘‘Rais Salva Kiir jana ametuma barua kwa mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa Ellen Loj akiahidi kwamba utawala wake utafanya uchunguzi wa tukio lililosababisha vifo vya walinda amani. Nazitaka mamlaka za Sudan Kusini hili lisicheleweshwe.’’