Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake ukanda wa maziwa makuu wakutana kujadili amani

Wanawake ukanda wa maziwa makuu wakutana kujadili amani

Wanachama wa jukwaa la amani, usalama na mashirikiano ( PSC) na mkakati wa makubaliano kwa ajili ya jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC na katika ukanda , wamekutana mjini Goma, mashariki mwa DRC, kuimarisha nafasi yao katika utekelezaji wa mkakati wa usalama na amani.

Mkutano huo wa siku mbili umelenga kuimarisha mkakati wa azimio la baraza la usalama la Umoja wa Mataifa namba 1325 linalohusu utatuzi wa migogoro na ujenzi wa amani katika ukanda wa maziwa makuu barani Afrika.

Jukwaa hilo linakusudia kuhakikisha wanawake katika nchi hizo ambazo ni Burundi, DRC, Rwanda na Uganda wanajihusisha katika jukumu muhimu la jitihada za amani katika ukanda wa maziwa makuu.

Mkutano huo umetoa fursa kwa ya kushirikisha uzoefu kuhusu namna gani jukwaa la wanawake limewasaidia kushiriki katika utatuzi wa migogoro na ujenzi wa amani katika jamii zao na kutoa mapandekezo kuhusu mustakabali wa jukwaa.