Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNCTAD 14 kufanyika Kenya ni kiashiria cha kukua kwa ushirikiano- Zewde

UNCTAD 14 kufanyika Kenya ni kiashiria cha kukua kwa ushirikiano- Zewde

Mkurugenzi Mkuu wa ofisi za Umoja wa Mataifa mjini Nairobi, Kenya, UNON Bi. Sewhle-Work Zewde amesema kufanyika kwa mkutano wa Umoja huo jijini humo ni kiashiria cha kuendelea kukua kwa uhusiano kati ya pande mbili hizo. Kutoka Nairobi Kenya, Assumpta Massoi na ripoti kamili.

(Taarifa ya Assumpta)

Nje ya jengo la ukumbi wa kimataifa wa mkutano la Kenyatta jijini Nairobi, Kenya, KICC harakati za kukabidhi jengo limekamilika...

Hatua hii imefanyika kwa kuteremsha bendera ya Kenya na kupandisha ile ya Umoja wa Mataifa yenye rangi ya buluu na nyeupe.

Nats..

Polisi wa Kenya walishusha bendera ya Kenya na wale wa Umoja wa Mataifa wakiwa wamevalia sare zao za buluu , wanasonga mbele kwa gwaride....

Taratibu, mmoja wao anakunjua bendera ile... anaipandisha...

(fx)

Sahle-Work  Zewde,Mkurugenzi Mkuu wa UNON ndiye mgeni rasmi na akafunguka..

(Sauti ya Sahle-Work)

"Kwanza kabisa inadhihirisha kiwango cha ushirikiano tulicho nacho na serikali ya Kenya. Na unafahamu Kenya ni mwenyeji wa mkutano wa 14 wa UNCTAD na imetukabidhi jengo hilo na kwamba ni kiashiria kuwa kando ya majengo yetu tuliyo nayo hapa Kenya, tunaweza kupeleka shughuli zetu kwingineko. Na kwangu mimi ni siku kubwa na inaonyesha kasi ya kukua kwa ushirikiano."