Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uganda na Djibouti wameshindwa kutimiza wajibu wao kumkamata Al Bashir: ICC

Uganda na Djibouti wameshindwa kutimiza wajibu wao kumkamata Al Bashir: ICC

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC imesema serikali ya Uganda na Djibout zimeshindwa kutekeleza ombi la mahakama hiyo la kumkamata na kumkabidhi Rais wa Sudan Omar Al Bashir kwa mahakama hiyo alipokuwa katika nchi zao.

Kwa ajili hiyo ICC sasa inalipeleka suala hilo kwa baraza la nchi zilizoridhia mkataba wa Roma na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa ,ili wachukue hatua zinazostahili kuhusiana na suala hilo la Uganda na Djibouti.

Rais Omar al Bashiri anakabiliwa na vibali viwili vya kukamatwa vya ICC kwa makossa matano ya uhalifu dhidi ya ubinadamu, mawili ya uhalifu wa vita na matatu ya mauaji ya