Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Walinda amani wawili wauawa kwa bahati mbaya wakati wa mafunzo Mali

Walinda amani wawili wauawa kwa bahati mbaya wakati wa mafunzo Mali

Walinda amani wawili wa Umoja wa mataifa wameuawa nchini Mali baada ya bomu kulipuka kwa bahati mbaya wakati wa zoezi la mafunzo.

Mpango wa Umoja wa mataifa nchini Mali MINUSMA,umesema tukio hilo limetokea wakati wa zoezi la kulenga shabaha mjini Kidali Kaskazini Mashariki mwa Mali siku ya Jumatano Asubuhi.

Mlinda amani wa tatu alijeruhiwa na anapatiwa matibabu kwa sasa. MINUSMA imeanza uchunguzi wa tukio hilo na duru za habari zinasema walinda amani hao wawili waliopoteza maisha walikuwa Raia wa Uholanzi.