Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu 350,000 wanahitaji chakula Swaziland:WFP

Watu 350,000 wanahitaji chakula Swaziland:WFP

Nchini Swaziland,watu 350,000 au theluthi moja ya watu wote nchini humo wanahitaji msaada wa chakula limesema shirika la mpango wa chakula duniani WFP.

Njaa inaongezeka katika taifa hilo la Kusini mwa afrika kutokana na ukame uliokithiri kwenyue ukanda mzima kwa zaidi ya miongo miwili sasa.

Msaada wa chakula wa WFP na msaada wa fedha vinatarajiwa kuwafikia watu 100,000 mwezi Agosti.

Serikali imetangaza hali tahadhari mwezi Febriari na kuzindua ombi la dola milioni 85 fedha za mpango wa dharura.