Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waharibifu CAR wanatumia ghasia:Onanga-Anyanga

Waharibifu CAR wanatumia ghasia:Onanga-Anyanga

Juhudi za kikatili za wale wanaojulikana kama waharibifu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, ambao wanaamua kutumia ghasia za silaha kutatua migogoro zimelaaniwa vikali na afisa wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa nchini humo.

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu, Parfait Onanga-Anyanga, amesema kumekuwa na matukio kadhaa ya ghasia katika wiki za karibuni kwenye sehemu mbalimbali nchini humo, matukuio ambayo yameleta bughdha na kukatili maisha ya watu pasi lazima, huku wengi wakijeruhiwa na kughubikwa na ukiwa.

Onanga-Anyanga amelaani vikali mashambulizi hayo , lakini akaongeza kwamba hayakuwa tishio la moja kwa moja la amani na juhudi za kuleta utulivu.