Skip to main content

Tutaendeleza ushirikiano ili kusambaratisha FDLR na ADF -MONUSCO

Tutaendeleza ushirikiano ili kusambaratisha FDLR na ADF -MONUSCO

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO umesema ushirikiano kati yao na vikosi vya serikali mashariki mwa nchi utaendelea hadi hatimaye kusambaratisha waasi.

Naibu Mkuu wa MONUSCO anayehusika na utawala wa sheria, David Gressly amesema ushirikiano huo umeanza kudhibiti vikundi vya waasi vya ADF na FDLR na kwamba..

(sauti ya David)

“Kwa hakika tunashughulikia kwa kina jambo hilo sasa, na tutaendelea bila kusita dhidi ya vikundi hivi vilivyojihami. Ninaamini hatimaye tutapata suluhusho la kudumu dhidi ya kitisho hiki.”

Amesema hivi sasa jambo muhimu ni..

(Sauti ya David)

“Tuna uwezo ambao upo ndani ya jeshi la DR-Congo na ushirikiano wa pande hizo mbili utakuwa na tofauti kubwa kwa maoni yangu.”