Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kinga ya surua ni muhimu kwa wakimbizi wa ndani Sudan Kusini:UNICEF

Kinga ya surua ni muhimu kwa wakimbizi wa ndani Sudan Kusini:UNICEF

Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, limesema ni muhimu sana kuwankinga watoto na surua katika kambi za wakimbizi wa ndani Sudan Kusini.

Kwa mujibu wa Afisa mawasiliano wa UNICEF Kim Owen, hii ni kwa sababu kambi hizo zimefurika, na surua ni maradhi yanayoambukiza, na hivyo watoto wako kwenye hatari kubwa ya kupata ugonjwa huo.

UNICEF imeanza kampeni rasmi ya kutoa chanjo hiyo, ikidhamiria kuwachanja watoto 13,000 kwenye kambi mbalimbali za wakimbizi wa ndani kweny mji wa Wau.