Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Matumizi ya samaki duniani yaongezeka:FAO

Matumizi ya samaki duniani yaongezeka:FAO

Matumizi ya samaki duniani yameongezeka zaidi ya kilo 20 kwa mwaka kwa mara ya kwanza, imesema ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo duniani, FAO.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyochapishwa leo ongezeko hilo la matumizi ya kila mtu yanatokana na usambazaji imara wa samaki na mahitaji ya baadhi ya aina za samaki, sanjari na uhifadhi wa samaki hao.

Hata hivyo FAO inasema licha ya hatua hizo kubwa lakini bado raslimali za majini hazijaimarika, na takribani theluthi moja ya akiba ya samaki wa biashara sasa wanavuliwa katika kiwango kisicho endelevu ikiwa ni mara tatu zaidi ya ilivyokuwa 1974.

Kimataifa ripoti inasema sekta ya uvuvi mwaka 2014 tani milioni 93.4 za samaki zilivuliwa.Manuel Barange ni mkurugenzi wa FAO kitengo cha sera na rasilimali za uvuvi, anafafanua juu ya ongezeko hilo la matumizi ya samaki

(SAUTI YA MANUEL)

"Watu milioni 57 walishiriki uvuvi kama kazi ya msingi, wengi wakiwa bara Asia na uuzaji wa samaki umepanda hadi dola bilioni148. Muhimu ni kwamba mauzo ya dola bilioni 80 ni kutoka nchi zinazoendelea kwa hiyo samaki sio tu chakula kwa jamii hizi bali pia inaongeza kipato cha kitaifa cha mauzo ya nje."