Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Shambulio karibu na msikiti Medina, ni shambulio dhidi ya dini:UM

Shambulio karibu na msikiti Medina, ni shambulio dhidi ya dini:UM

Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa mataifa Zeid Raad Al-Hussein, amelaani shambulio la bomu lililotokea Jumatatu karibu na msikiti wa mtume mjini Media Saudia.

Amesema Medina ni moja ya mahalai patakatifu kwa Uislamu na kwa kutokea shambulio kama hilo wakati wa mfungo wa Ramadhan , kunaweza kuchukuliwa kama ni shambulio dhidi ya Waislamu kote duniani.

Amesema athari za shambulio hilo sio tuu kwa polisi wanne waliopoteza maisha na uharibifu , bali ni shambulio kwa dini yenyewe na ni kitu kisichokubalika.

Kumearifiwa pia kuwepo na mashambulizi mengine mawili ya bomu kwenye ufalme wa Saudia mjini Qatif na Jeddah.