Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Akiwa Israel, Ban akutana na Rais Rivlin; apokea medali

Akiwa Israel, Ban akutana na Rais Rivlin; apokea medali

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, leo ametua nchini Israel, akiendelea na ziara yake Mashariki ya Kati. Akiwa Israel, Ban amekutana na Rais wa Israel Reuven Rivlin, Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu.

Baadaye akikutana na wanahabari akiwa ameandamana na Rais Rivlin, Ban amesema vitendo vya ghasia baina ya Waisraeli na Wapalestina, mathalan udungaji visu, ufyatulianaji risasi na mashambulizi ya mabomu, havitaleta ufanisi wowote.

Amesema ghasia daima haziwezi kuwa suluhu, akiongeza kuwa vitendo kama hivyo vinalenga tu kuzua hofu na sintofahamu, na kuwatenganisha Waisraeli na Wapalestina hata zaidi.

Aidha akiwa Israel, Ban ametembelea Chuo Kikuu cha Tel Aviv, ambako amepewa medali ya George S. Wise.