Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Myanmar yaathiriwa na mafuriko:UM

Myanmar yaathiriwa na mafuriko:UM

Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa na mratibu wa masula ya kibinadamu hususani mafuriko nchini Myanmar, Janet Jackson amesema majimbo mengi nchini humo yamethiriwa pakubwa na mvua nyingi zinazoendelea tangu mwanzoni mwa mwezi Juni.

Katika taarifa yake amesema kwa mujibu wa idara ya masuala ya usaidizi wa kibinadamu na makazi ya serikali, takribani watu 26,000 wameathirwa na huku watu 14 wakiripotiwa kufariki.

Bi Jackson ametuma salamu za pole kwa wanafamilia na jamii waliotahiriwa na mafuriko hayo yaliyoathiri zaidi ya nyumba 5,000 huku nyingine zaidi ya 200 zikiharibiwa.

Amesema Umoja wa Mataifa uko tayari kutoa usaidizi kwa serikali na watu wa Myanmar