Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkakati wa nishati endelevu kwa Wote waongeza kasi

Mkakati wa nishati endelevu kwa Wote waongeza kasi

Mkakati wa nishati endelevu kwa Wote sasa unaongeza kasi kwa mchakato mpya wa miaka mitano unaolenga kuchochea hatua za kutimiza ahadi zilizowekwa katika malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) na Mktaba wa Paris kuhusu tabianchi.

Muundo mchakato huo wa “Songa mbele, Haraka”, ambao unalenga kuleta mafanikio kati ya mwaka 2016-2021, umeungwa mkono leo na viongozi waandamizi kutoka bodi ya Nishati Endelevu kwa Wote, ambayo wenyekiti wenza wake ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon na Rais wa Benki ya Dunia, Jim Yong Kim.

Katibu Mkuu Ban Ki-moon amesema nishati safi na yenye gharama nafuu ndicho kiungo muhimu zaidi cha ukuaji wa kiuchumi, kuongeza usawa katika jamii na kutunza mazingira, akiongeza kuwa kuna haja ya kuwekeza mabilioni ya dola za ufadhili, ili kuweza kutimiza matamanio ya kuwa na nishati endelevu na nafuu.

Hata hivyo, Ban amesema hilo litawezekana tu kupitia ubia vumbuzi wa sekta za umma na sekta binafsi, pamoja na uchagizaji uwekezaji.