Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nguli wa mitindo Kenneth Cole awa balozi mwema UNAIDS

Nguli wa mitindo Kenneth Cole awa balozi mwema UNAIDS

Shirika la Umoja wa mataifa linalohusika na masuala ya ukimwi UNAIDS limemteua mwenyekiti wa amfAR na mbunifu maarufu wa mitindo duniani Kenneth Cole kuwa balozi mwema wa shirika hilo.

Tangazo hilo limetolewa leo katika tukio maalumu lililofanyika makao makuu ya Umoja wa Mataiga katika kuelekea mkutano wa baraza kuu utakaoaanza kesho Jumatano Juni 8 hadi 10, kwa lengo la kutokomeza ukimwi.

Akizungumzia uteuzi huo mkurugenzi mkuu wa UNAIDS Michel Sidibe amesema dunia inaingia katika awamu muhimu sana ya vita dhidi ya ukimwi na anajua Kenneth atakuwa na mchango mkubwa katika mtazamo wa pamoja wa kutokomeza ukimwi ifikapo 2030, na kuongeza.

image
Michel Sidibe.(Picha:UM/Mark Garten)
(SAUTI YA MICHEL SIDIBE)

““Tunapozungumzia kupambana na ugonjwa wa ukimwi, ninaangalia mtu mwenye shauku na huruma, najaribu kuhakikisha kwamba huyu mtu ana moyo na anajaribu kuchangamana na idadi kubwa ya watu. Anaweza kuwa mtu kutoka ngazi ya jamii au anaweza kuwa Kenneth Cole, na kwa hili nimefurahi sana kwamba ni Kenneth kwa sababu Kenneth ni mtu wa watu, amekuwa akipambana wakati wote kuhakikisha kwamba tunavunja unyanyapaa, ubaguzi na pia amekuwa akitia shime kupata tiba”

Bwana Cole amekuwa mwanaharakati anayepaza sauti katika vita vya kimataifa dhidi ya ukimwi kwa zaidi ya miaka 30 na anaendelea na dhamira hiyo ya kuwapigia upatu watu wanaoishi na VVU.Akizungumza baada ya kutangazwa kwakwe rsmi kama balozi mwema amesema kilichomsukuma kukubali jukumu hilo ni Michel Sidibe hasa

(SAUTI YA KENNETH COLE)

“Maono yake, uongozi wake, uwezo wake na huruma yake ya kuwaweka watu mbele, kujikita kwakwe katika kupigania haki za binadamu na utu wake ni suala la kujivunia. Hivyo nikavutia kutaka kusikia , kuelewa na kujifunza zaidi”

image
Kenneth Cole.(Picha:UM/Mark Garten)
Pamoja na kujikita katika biasahara ya masuala ya mitindo, ni mwenyekiti wa mfuko wa amfAR unaohusika na utafiti kuhusu ukimwi tangu mwaka 2005.

Cole amekuwa kinara wa kampeni ya karibuni ya amfAR ya kusada tiba ambapo imefungua taasisi ya utafiti wa HIV katika chuo kikuu cha California, San Francisco. Lengo la taasisi hiyo ni kuchagiza mchakato wa kuelekea kutengeneza tiba ya ukimwi.