Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Miaka 5 ya vita Kordofan Kusini watu bado wafunjgasha virago:UNHCR

Miaka 5 ya vita Kordofan Kusini watu bado wafunjgasha virago:UNHCR

Mwishoni mwa wiki hii itakuwa ni majuma matano tangu kuzuka kwa vita kwenye jimbo la Kordofan Kusini nchini Sudan.

La kusitikisha zaidi,  watu hadi leo hii bado wanafungasha virago na wengi wao wanavuka mpaka na kukimbilia nchi jirani ya Sudan Kusini limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR.

Hadi sasa , mwaka 2016 zaidi ya wakimbizi 7500 wamewasili Yida Sudan Kusini jimbo la Unity, ambako tayari ni maskani ya wakimbizi wengine 7000. Adrian Edward ni msemaji wa UNHCR

(Sauti ya Adrian Edward)

"Upatikanaji wa huduma muhimu uko mashakani huku huduma ya maji ikipungua, aidha shule zimerundikana watoto, huku darasa moja likiwa na zaidi ya watoto mia moja. Ufadhili wa Sudan Kusini ni asilimia 17 tu katika taifa lenye wakimbizi takiribani milioni 1.7 waliofurushwa makwao."